Jumamosi , 4th Aug , 2018

Timu ya Kikapu ya Portland imefanikiwa kushinda game 2 ya nusu fainali ya michuano ya Sprite Bball Kings dhidi ya Mchenga Bball Stars hivyo kulazimisha kucheza game 3 ili kupata mshindi atakayekwenda fainali.

Mechi kati ya Mchenga Bball Stars dhidi ya Portland.

Katika mchezo huo uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa taifa wa ndani, Portland wameshinda pointi 71 dhidi ya 64 za Mchenga Bball Stars ambao ndio mabingwa watetezi.

Shukrani za pekee kwa mashabiki wa Portland zitamwendea nyota wao Denis Babu ambaye amefunga pointi 24, na kuchukua rebound 7 na Assist 2. Hivyo Babu amewaokoa kutoaga mashindano kwenye game 2.

Kwa upande wa Mchenga Bball Stars wao leo wameongozwa na nyota wao Baraka Isack ambaye amefunga pointi 22, rebound 3 na Assist 2, japo zimeshindwa kuisadia timu yake kwenda fainali bila kucheza game 3.

Katika game 1 Mchenga Bball Stars walishinda kwa pointi 70 kwa 54. Portland sasa zitacheza game 3 ili kumpata mshindi atakayekwenda fainali kuwania milioni 10 akiwa bingwa au milioni 3 akiwa wa pili pamoja na milioni 2 kwa atakayekuwa MVP.