Hayo yamethibitishwa mnamo Novemba 19,2023 na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa katika mapokezi ya timu ya Taifa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambapo ametumia nafasi hiyo kusema kuwa Stars itaishangaza Dunia kwa kuifunga Morocco huku akiwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Benjamin Mkapa Novemba 21,2023.
Jumatatu , 20th Nov , 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amenunua tiketi zote za mzunguko kwa ajili ya kuwapatia Watanzania fursa ya kwenda uwanjani kuipa hamasa timu ya Taifa 'Taifa Stars' kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kombe la Dunia 2026 dhidi ya Morocco kesho jumanne.