Kikosi cha Yanga SC kilichoanza dhidi ya Simba SC Julai 3, 2021.
Takwimu hizi ni katika michuano ya Ligi Kuu soka Tanzania bara ambapo kati ya hizo 12, Yanga imeshinda mara 4, sare 5 huku Simba SC wakishinda mara tatu.
Kabla ya mechi ya jana ambayo ilikuwa ya mzunguko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2020-21 timu hizo zilikuwa zimekutana mara 11 huku kila timu ikishinda mara 3 na sare mara 5.
Goli pekee la mchezo wa jana uliopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa na kushuhudiwa na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, lilifungwa na Zawadi Mauya dakika ya 12 na kuifanya Yanga kufikisha pointi 70 katika michezo 32, ikiwa nyuma ya Simba SC yenye pointi 73 katika mechi 30.
Timu hizo zitakutana tena Julai 25, 2021 kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma kwenye mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho nchini.




