Jumanne , 14th Jul , 2020

Klabu ya soka ya Real Madrid itatwaa ubingwa wa ligi kuu ya Hispania iwapo itaifunga Villarreal siku ya Alhamis katika mechi ambayo itawahakikishia wanamaliza juu ya mabingwa watetezi wa La Liga, Barcelona.

Karim Bemzema wa kwanza kushoto (Pichani) akishangilia bao na wenzake katika mchezo wa Jumatatu dhidi ya Granada.

Los Blancos inahitaji alama mbili pekee ili itwae taji lake la 34 la La Liga,baada ya usiku wa Jumatatu kuinyika Granada bao 2-1 ikiwa ugenini na kufikisha alama 83 na kuiacha Barcelona wenye alama 79 wakiwa wamesalia na mechi tatu kila mmoja.

Mabao ya Real Madrid yalifungwa na Phelan Mendy dakika ya 10 na Karim Bemzema dakika ya 16 wakati bao la kufutia machozi la Granada lilifungwa na Darwin Machis dakika ya 50 ya mchezo.

Vijana wa kocha Zinedine Zidane walipata ushindi wa tisa mfululizo tangu kurejea kwa ligi baada ya mapumziko ya dharula yaliyosababishwa na COVID-19 na wanakaribia kuwavua ubingwa Barcelona ambao hata wakishinda mechi zote zilizosalia na Madrid wakainyuka Villarreal haitowasaidia.

Iwapo Real Madrid itafanikisha kutwaa La Liga siku ya Alhamis, itampa nafasi kocha Zinedine Zidane kukiandaa kikosi chake na mechi ya marudiano dhidi ya Manchester City ambao ni wa hatua ya 16 bora dhidi ya Manchester City ,ligi ya mabinga Ulaya ambao wako nyuma kwa bao 2-1.