Jumamosi , 19th Sep , 2020

Bayern Munich ameweka rekodi kwa kuwa timu pekee kupata ushindi mkubwa katika mchezo wa ufunguzi wa Bundesilga baada ya kuichapa Schalke 04 bao 8-0.

Serge Gnabry(Pichani) ndiye aliyefunga magoli matatu peke yake wakati Bayern Munich ikiiadhibu vilivyo Schalke 04 katika ufunguzi wa Bundesilga.

Serge Gnabry alifunga magoli matatu, Leon Goretzka, Roberto Lewandowski,Thomas Muller,Leroy Sane na Jamali Musiala ndio waliopeleka maangamizi kwa upande wa Schalke 04 usiku wa jana .

The Bavarians pia wameweka rekodi nyingine ya kushinda mechi 30 mfululizo na sare 1 tangu wafungwe disemba mwaka jana.

Kocha Hans Flick ameshinda mechi 22 mfululizo hadi hivi sasa.

Kikosi  cha kocha Hans Flick kimepata ushindi wa pili mkubwa ndani ya mwaka huu,waliinyuka Barcelona katika nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya kwa bao 8-2.

 

Kwa upande wa Schalke wameendelea kuwa na mwenendo mbaya,hawajashinda mchezo wa Bundesilga tangu Januari 17 mwaka huu,na wamepoteza mechi 7 kati ya 9 walizocheza.

TAKWIMU KALI

-Bayern Munich Na Schalke 04 Zimekutana Mara 100 Katika Bundesilga.

-Bayern ilikutana na Schalke 04 kwa mara ya 101 katika bundesilga jana na wakaipa kichapo cha aina yake cha bao 8-0 na kuandikisha takwimu mbali mbali za kuvutia.

Katika mechi 101

-Bayern imeshinda 55
-Schalke imeshinda 18
-Sare 28
.
Katika Mechi 10 za Mwisho Walizokutana
-Bayern Kashinda Zote 10
-Bayern Kafunga Bao 30 Na Kuruhusu Bao 2 pekee.

Katika mchi 20 za mwisho;

-Bayern kashinda mechi 18 na sare 2 tu
-Robert Lewandowski alifunga bao 34 msimu Uliopita katika Bundesilga,,sasa amefunga bao lake la kwanza msimu huu na ikumbukwe alifunga bao 55 katika mechi 27 za mashindano yote msimu uliopita.

-Robert Lewandoski Alifunga bao 4 Kati ya magoli 5 Ambazo Bayern Iliifunga Schalke Katika Mechi 2 walizokutana msimu uliopita,jana kafunga tena .
.
Kwa kufunga jana dhidi ya Schalke 04,Vilevile Robert Lewandoski ameifunga timu hiyo goli 20 katika mechi 20 alizokutana nao.