Jumatano , 2nd Feb , 2022

Nusu fainali ya kwanza ya michuano ya soka ya mataifa barani Afrika AFCON inachezwa leo usiku ambapo timu ya taifa ya Burkina Faso na Senegal zitashuka dimbani kuchuana kuwania nafasi ya kucheza fainali ya michuano hii.

Wachezaji wa timu ya taifa ya senegal wakishangilia goli kwenye moja ya michezo ya AFCON

Mchezo huu unachezwa katika uwanja wa Ahmadou Ahidjo huko Yaounde Cameroon na mtanange huu utachezwa kuanzia Saa 4:00 usiku.

Timu zote mbili hazijawahi kutwaa ubingwa wa AFCON, Senegal wamecheza fainali mbili za michuano hii na zote wamepotea walicheza fainali ya kwanza mwaka 2002 walifungwa kwa mikwaju ya penati 3-2 dhidi ya Cameroon na mwaka 2019 walifungwa bao 1-0 na Algeria.

Burkinafaso ambao pia ni washindi wa 3 wa fainali zilizopita  za mwaka 2019 wanaiwinda fainali ya pili baada ya kucheza fainali yao ya kwanza kwenye michuano hii mwaka 2013 fainali ambayo walipoteza kwa kufungwa bao 1- 0 na timu ya taifa ya Nigeria.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Burkina Faso

Na katika michezo 12 waliokutana Senegal wameshinda mara 3 Burkina Faso mara 2 na michezo 7 imemalizika kwa sare. Burkinafaso chini ya kocha Kamou Malo imefungwa mchezo 1 tu kwenye michezo 11 ya mwisho kwenye michuano yote, wakati kocha Aliou Cisse wa Sengal hajapoteza mchezo kwenye michezo 11 ya mwisho kwenye michuano yote kashinda michezo 8 na sare michezo 3.