
Kaimu Afisa abari wa klabu ya Simba, Ezekiel Kamwaga.
Kamwaga amesema, “Kuhusu kambi ya Simba iliyopo Morocco huko kila kitu kinakwenda sawa kuanzia kwa wachezaji wenyewe wanasema kuwa kambi ni nzuri”. Simba ipo nchini Morocco kwa kambi ya siku 14 ambapo tayari wameshafikisha siku 6 tokea wafike nchini humo.
Licha ya maendeleo mazuri ya kambi hiyo, Simba bado haijathibitisha ni lini hasa watacheza mchezo wa kirafiki nchini humo kama eneo la kuweka sawa utimamu wa wahezaji wake.
Kwa upande mwingine Kamwaga amejibia suala la mashabiki kuulizia upatikanaji wa jezi mpya wa wekundu hao wa msimbazi kwa kusema kuwa, wanategemea kutambulisha jezi hiyo kuanzia wiki ijayo kabla ya tamasha la siku ya Simba 'Simba day'.
“Mzigo wa jezi upo na tutautambulisha wiki moja kabla ya siku ya Simba day. Mambo yanakwenda vizuri na kuanzia msimu ujao tutafanya kwa uzuri zaidi” alisema Kamwaga.
Simba imewajumisha wachezaji wake wapya waliowasajili kwenye dirisha hili kubwa la usajili ambao ni Duncan Nyoni, Peter Banda, Israel Patrick Mwenda, Abdulsamad Ally Kassim na Henock Inonga Banda.