
Rooney ambaye anaongoza rekodi ya ufungaji wa muda wote ametajwa katika kikosi cha wachezaji 26 kwa ajili ya michuano ya Euro 2016.
Shearer amesema Rooney mwenye miaka 30 anafaa zaidi katika nafasi ya kiungo nyuma ya Harry Kane na Jamie Vardy. Ameongeza kuwa ni lazima pawepo nafasi kwa ajili ya nahodha wa timu na amefurahi imepatikana.
Siku za Wayne Rooney kuwa mshambuliaji wa kwanza zimeisha. Harry Kane na Jamie Vardy wanapaswa kuanza mbele lakini bado Rooney ana nafasi kubwa ya kucheza kama namba kumi kama kiungo wa kati, alisema Shearer.
Rooney ni miongoni mwa washambuliaji watano walioitwa katika kikosi cha Roy Hodgson siku ya Jumatatu kwa ajili ya michuano ya Euro 2016. Wengine ni Harry Kane, Jamie Vardy, Daniel Sturridge na Dogo Marcus Rashford.