Jumanne , 17th Jun , 2014

Chama cha Riadha nchini RT kimesema pamoja na changamoto ya ukata unaokikabili chama hicho wao kama chama wanaendelea na maandalizi ya michuano ya taifa yatakayofanyika jijini Dar es salaam.

Wanariadha wakichuana katika moja ya michuano ya taifa.

Chama cha Riadha Tanzania RT kimesema maandalizi ya michuano ya riadha ya taifa itakayofanyika jijini Dar es salaam kwa siku mbili kuanzia Julai 12 hadi 13 mwaka huu yanakwenda vizuri japo chama hicho kinakabilana na changamoto ya ukata wa fedha za kuwezesha mashindano hayo kufanyika kwa ufanisi na ubora zaidi

Katibu mkuu msaidizi wa chama cha riadha Tanzania RT Ombeni Zavara amesema RT inafanya maandalizi ya michuano hiyo mikubwa ya taifa ikiwa na ukata wa fedha hivyo amewaomba wadau na makampuni mbalimbali kujitokeza kusaidia ili kuweza kufanikisha michuano hiyo

Aidha Zavara amesema chakusikitisha zaidi ni mpaka sasa siku zikiwa zinazidi kusogea hakuna hata mkoa mmoja uliothibitisha ushiriki wa michuano hiyo huku pia akiwataka wanaridaha wanaotaraji kushiriki michuano hiyo kuhakikisha wanajianda vema na michuano hiyo.