Ijumaa , 27th Jan , 2023

Klabu ya Ruvu Shooting imesema haridhishwi na mwenendo wa matokeo mabaya wanayoyapata hadi kuwafanya washike mkia kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC Tanzania msimu huu wa mwaka 2022-23 kwa kuwa na alama 14 baada ya kucheza

Afisa Habari wa klabu ya Ruvu Shooting Stars, Masau Bwire amesema upinzani mgumu uliopo kwenye Ligi kuu  NBC Tanzania unawafanya wapate tabu lakini wameahidi kupambana zaidi kwani wanaimani watarejea kwenye ubora wao na kusalia ligi Kuu.

“Tuko kwenye nafasi mbaya na hatujaridhishwa kuwa katika nafasi huyo kwa sababu sio nzuri kabisa na kamwe hakuna mtu anayeridhishwa na kitu kisicho kizuri hivyo tutazidi kupambana.

“Kushindwa kupata matokeo mazuri haina maana ya kuwa timu haijitumi au shida ipo kwa walimu wao ila inatokea hivo kwa sababu ya ligi kuwa ngumu na kuwa ya ushindani wa hali ya huu hivyo kila timu inahitaji kupata ushindi ili iwe katika nafasi nzuri,” amesema Bwire.

Kwenye msimamo wa ligi kuu Ruvu Shooting inayoshika mkia ikiwa na alama 14 inahitaji kufikisha alama 23 itoke kwenye hatari ya kushuka daraja au ipate alama 6 ambazo zitawaweka kwenye nafasi ya 13 nafasi ambayo itamuwezesha kucheza michezo ya ‘Playoff’ kuwania kusalia hiyo..