(Kutoka kushoto: Dele Alli, Dan Burn na Pierre-Emerik Aubameyang)
Mshambuliaji huyo aliyekuwa tegemezi kwenye kikosi cha washika mitutu Jijini Londo, alikutwa na kosa la kinidhamu kwa mara ya pili na Kocha wake Mikel Arteta akaamua kumsimamisha tokea Disemba 6 ambapo hakucheza tena.
Aubameyang alifanikiwa kucheza michezo 163, kufunga mabao 92 na kutengeneza mengine 20 ambayo yalisaidia kuifanya Arsenal kubeba Ubingwa wa FA CUP na Kombe la fainali ya Ngao ya Hisani ya Jamii.
Kwa Upande mwingine,
Aliyekuwa Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Hotspurs ‘Masharobaro wa Jiji la London’, Dele Alli amekamilisha usajili wa kujiunga na Everton kama mchezaji Huru na kusaini kandarasi ya miaka miwili na nusu.Dele Alli alipoteza namba kwenye kikosi cha kwanza cha Spurs baada ya kuwa nje kwa majeraha ya muda mrefu na pindi aliporejea hakuweza kupata nafasi kwa kocha Jose Mourinho hivyo ameamua kutafuta nafasi ya kucheza zaidi.
Spurs pia imewasajili viungo, Rodrigo Bentancur kwa kandarasi ya miaka miwili pamoja na Dejan Kulusevski kwa mkopo wote kutoka Juventus kuziba nafasi za Tanguy Ndombele aliyeenda Lyon, Bryan Gil kwenda Valencia na Giovani Lo Celso kwenda Villarreal wote watatu kwa Mkopo.
Beki wa kati Dan Burn amejiunga na Newcastle United akitokea Brighton & Hove Albion. Burn amerejea Newcastle Kwenye timu yake ya utotoni aliyoichezea akiwa bwana mdogo wa miaka 11 na sasa ana miaka 29.
Naye kiungo mshambuliaji wa zamani wa Spurs na Inter Milan, Christian Eriksen amejiunga na Brentford kwa dau ambalo halikuwekwa wazi. Kumbuka Eriksen alisitishiwa mkataba wake na Inter Milan baada ya kugundulika na matatizo ya moyo.
Sheria za Serie A haziruhusu mchezaji kucheza akiwa na kifaa cha kumsaidia kupumua kwenye moyo wake utaratibu amabo ni kinyume na nchini England.





