Jumanne , 22nd Oct , 2019

Mshambuliajiwa KRC Genk, Mbwana Samatta atakuwa katika wakati mzuri wa kuonesha uwezo wake mbele ya mabingwa watetezi wa michuano ya Klabu Bingwa Ulaya, Liverpool baada ya safu yao ya ulinzi kupungua nguvu.

Samatta na mabeki wa pembeni wa Liverpool

Mchezo huo wa tatu hatua ya makundi unatarajia kupigwa leo Jumatano katika uwanja wa Luminius Arena mjini Genk, nchini Ubelgiji, ambako ndiyo maskani ya klabu hiyo anayokipiga nahodha wa Taifa Stars.

Taarifa zilizopo hii zinaeleza kuwa mlinzi machachari wa upande wa kulia wa Liverpool, Trent-Alexander Anold hajafanya mazoezi na klabu yake kutokana na kukumbwa na homa, hivyo hatokuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza dhidi ya Genk.

Genk ya Mbwana Samatta iko katika kundi E ikiwa na pointi moja katika nafasi ya mwisho baada ya kufungwa mechi moja na kutoka sare mechi moja. Napoli inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi 4, huku Liverpool ikiwa na pointi 3 katika nafasi ya pili na Red Bull Salzburg ikiwa katika nafasi ya tatu kwa pointi 3.

Matokeo ya michezo iliyopigwa usiku wa jana ni Club Bruge 0-5 PSG, Galatasaray 0-1 Real Madrid, Olympiakos 2-3 Bayern Munich, Tottenham 5-0 Red Star Belgrade, Shakhtar Donetsk 2-2 Dinamo Zagreb, Man City 5-1 Atalanta, Atletico Madrid 1-0 Bayer Leverkusen, Juventus 2-1 Lokomotiv Moscow.

Michezo itakayopigwa leo ni Ajax Vs Chelsea, RB Laeipzig Vs Zenit, Slavia Praha Vs Barcelona, Red Bull Vs Napoli, Genk Vs Liverpool, Inter Milan Vs Dortmund na Benfica Vs Lyon.