Alhamisi , 15th Sep , 2016

Nahodha wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta, leo anatarajiwa kuiongoza tena KRC Genk katika mchezo wa kwanza wa Kundi F la Europa League dhidi ya wenyeji, Rapid Vienna nchini Austria.

Mbwana Samatta, katika moja ya michezo na klabu yake ya Genk

Samatta amesema wamepangwa kundi gumu tofauti na watu wanavyofikiria.

Mchezo mwingine wa kundi hilo, Sassuolo ya Italia watakuwa wenyeji wa Athletic Bilbao ya Hispania katika Uwanja wa Citta.

Kwa upande wa kundi A, Manchester United itakuwa ugenini nchini Uholanzi kuvaana na Feyenoord.