Jumanne , 28th Sep , 2021

Fainali za Ligi ya kikapu jijini Dar es Salaam ‘RBA’ mwaka 2021 zinataraji kuendelea kuanzia jioni ya leo Septemba 29, 2021 kwa michezo miwili yote ya game 3.

Nyota wa zamani wa NBA akiwa na timu yake ya sasa ya Savio kwenye fainali za RBA 2021.

Timu ya Savio na timu ya Army Basketball Club ‘ABC’ zitakipiga tena saa 2:00 usiku wa leo kwenye uwanja wa Don Bosco Oystrebay jijini Dar es Salaam baada ya wawili hao kucheza game 2 Ijumaa iliyopita ambapo ABC ilishinda kwa alama 84 kwa 79 dhidi ya Savio na kufanya series ya fainali kuwa 1-1.

Gmae 3 inatazamiwa kuwa ya kukata na shoka kila upande ukihitaji kupata ushindi wa uongozi ili kujiandalia mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa RBA 2021 na mvuto ukizidi kutokana na viwango bora vya nyota wa Savio Hasheem Thabeet na Erenico Maengela wa ABC.

Hasheem ambaye ni mchezaji wa zamani wa NBA, alishwa moto na kufikisha alama 35, rebound 15, assist 4, kuzuia mipira mara 4 na kupora mmoja na kuibuka kuwa nyota wa mchezo wakati Erenico Maendela wa ABC alifikisha alama 27, rebound 8 na kupora mipira mara 2 na kuibuka kuwa nyota wa mchezo.

Kwa upande wa RBA ya Wanawake, JKT Stars inayoongoza series ya fainali hiyo kwa 2-0 dhidi ya Vijana Queens na wao watacheza saa 12:00 jioni ya leo kwenye game 3 katika uwanja wa Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam  na kama JKT Queens itapata ushindi kwenye game 3 basi watasaka ushindi mmoja mwingine ili kufikisha ushindi wa series 4-0 ili waweze kuwa mabingwa.