Jumatatu , 15th Feb , 2021

Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA)  Dkt. Mohammed Seif Khatib, amefariki dunia leo asubuhi Jumatatu Februari 15, 2021.

Dkt. Mohammed Seif Khatib

Mwanasiasa huyo Mkongwe, amewahi kuwa mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, Mbunge wa Uzini vipindi kadhaa, Waziri wa Wizara mbalimbali katika Serikali ya Muungano.

Aidha Khatib ambaye bado chanzo cha kifo chake hakijawekwa wazi, pia alikuwa mshairi, na mwandishi aliyechapisha vitabu kadhaa.

Pia amefanya kazi kama Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dodoma.

Kwa upande wa michezo amewahi kuwa mchezaji wa soka Kikwajuni Sports Club na timu ya Taifa ya Zanzibar.

Katika burudani Khatibu alikuwa Mwimbaji wa Taarab na kwenye biashara pia alikuwa mmiliki wa kituo cha Radio ya Zenj FM.