Jumatano , 15th Apr , 2015

Chama cha Mpira wa Magongo Mkoa wa Dar es salaam kimesema Programu ya kukuza michezo katika shule za msingi na Sekondari nchini imezidi kukua na wanaamini itasaidia kupata vipaji vipya.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu wa DRHA, Mnonda Magani amesema programu hiyo imezidi kusambaa ambapo kwa hapa Dar es salaam wanaendelea kutoa mafunzo hayo kwa shule ya Sekondari ya Kibasila huku mkoa wa Lindi wakianza na shule nne.

Magani amesema, Programu hiyo itazidi kuenea katika shule mbalimbali za mikoa ya hapa nchini huku wakiamini kwa kupitia Programu hiyo wataweza kupata walimu pamoja na wanamichezo bora hapa nchini watakaoshiriki na kushinda mashindano makubwa ya ndani na nje ya nchi.