
Wachezaji wa Mali (U-17) wa kikosi kilichotinga fainali ya Kombe la Dunia kwa vijana
Timu nyingine zilizo katika kundi hilo ni Niger pamoja na Angola
Fainali hizo ambazo awali zilipangwa kufanyika mwezi April mwaka huu nchini Madagascar, sasa zitafanyika kuanzia Mei 21 hadi Juni 4 mwaka huu nchini Gabon kuchukua nafasi ya Madagascar iliyopokonywa uenyeji mwezi uliopita baada ya kubainika kutotimiza vigezo.
Michuano hiyo itatoa timu nne ambazo zitaiwakilisha Afrika kwenye Kombe la Dunia la FIFA chini ya umri wa miaka 17 itakaofanyika nchini India baadaye mwaka huu. Niger walikuwa wenyeji wa Afcon iliyopita ya U-17 mwaka 2015 na Mali wakatwaa ubingwa.
Mali pia ilifanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Kombe la Dunia wa vijana U-17 ambapo ilifungwa na Nigeria
Makundi yote mawili yako kama hivi