Serengeti Boys waahidiwa milioni 20 kila mchezaji

Ijumaa , 12th Apr , 2019

Wachezaji wa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania, U-17 'Serengeti Boys' wameahidiwa kupewa Sh. 20 milioni kila mchezaji endapo watashinda mechi 2 za AFCON.

Serengeti boys

Ahadi hiyo imetolewa na Mlezi wa timu ya vijana Serengeti Boys Dkt.Reginald Mengi pamoja na Kamati ya kuhamasisha ushindi wa timu hiyo inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar, es salaam, Paul Makonda.

Michuano ya vijana ya AFCON inatarajia kuanza April 14, Tanzania ikiwa ni mwenyeji. 

Serengeti Boys inahitaji kushinda mechi mbili ili kujikatia tiketi ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia kwa vijana chini ya miaka 17 itakayofanyika nchini Brazil mwaka huu.

Michuano hiyo itafanyika katika viwanja viwili, ambavyo ni Uwanja wa Taifa na Uwanja wa Azam Complex Chamazi. Timu shiriki zimepangwa katika makundi mawili, ambapo kundi A lina timu za Tanzania, Nigeria, Angola na Uganda, huku kundi B likiwa na timu za Guinea, Cameroon, Morocco na Senegal.