Alhamisi , 24th Mar , 2016

Benchi la ufundi la timu ya Taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys, linatarij

Benchi la ufundi la timu ya Taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys, linatariji kuwa na mbinu za kuhakikisha timu hiyo inafuzu kuelekea fainali za Afrika nchini Madagascar mwaka 2017.

Kocha msaidizi wa timu hiyo Bakari Shime, amesema hawatokuwa na mpira wa kumfurahisha mtu, bali falsafa yao ni kucheza kwa ajili ya kufuzu fainali hizo, ambapo wakikabiliwa na mchezo wa kwanza dhidi ya timu ya Sheli Sheli mwezi juni mwaka huu.

Shime aliyekuwa kocha wa zamani wa Mgambo JKT, amesema siku zote mbinu ni ushindi na mpira wa chenga twawala hauna faida, hivyo watatumia falsafa ya ushindi ni muhimu.

Serengeti Boys,ipo chini ya kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars,Mdernmark, Kim Paulsen, ambaye amerejeshwa na TFF kuwa kocha wa timu za Taifa za vijana.

Kikosi cha Serengeti Boys kina jumla ya wachezaji 43, ambao wameanza kambi tangu jumatatu ya machi 21 mwaka huu kwenye hosteli za TFF, Karume jijini Dar es Salaam.

Vijana hao watakuwa na kambi ya wiki mbili, kabla ya kuanza mechi za kirafiki mwezi wa nne na wa tano, kuelekea mechi yao ya kufuzu dhidi ya Sheli Sheli mwezi Juni mwaka huu.