Jumanne , 14th Feb , 2023

Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo imepokea Hekari 12 eneo la Kawe Jijini Dar es salaam ambapo utajengwa Ukumbi wa Kimataifa wa Michezo (Sports Arena).

Akizungumza na Wanahabari Leo Februari 14,2023 Waziri wa utamaduni sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa amesema Watanzania wana kiu ya kuona Ukumbi wa Kimataifa wa michezo kama zilivyo nchi zingine unajengwa nchini Tanzania.

Hata hivyo Mchengerwa ameeleza kuwa Kujengwa kwa ukumbi huo utabeba watu zaidi ya elfu 16 ambapo Arena kubwa ipo nchini Senegal inachukua watu elfu 15.

"Arena yetu itachukua watu elfu 16 na tunategemea pia ichukue watu mpaka elfu 20 ili Watanzania wapate nafasi kushuhudia matamasha mengi katika ukumbi huo."

Hata hivyo Mchengerwa ameeleza kuwa dhamira ya Dkt.Samia Suluhu ni kuhakikisha Sekta ya burudani na Michezo zinakuwa  Sekta zinazokwenda Kuchangia pato la Taifa

"Watanzania wamekuwa wakihoji kuwa tayari bajeti imepitishwa lakini hawaoni utekelezaji wa ujenzi wa Ukumbi huo lakini tuwatoe hofu kuwa sasa tunaenda kuandika historia nchini Tanzania kujengwa kwa ukumbi huo wa Kimataifa."

Pia ameeleza Arena hiyo inatarajiwa kukamilika kwa miezi 08 hadi 10 ambapo utakuwa ukumbi wa Kimataifa barani Afrika. 

"Tulipotoka hatukuwa na mipango mizuri hivyo tulivoingia na wasaidizi wangu tumehakikisha tunaenda kuongeza nguvu kubwa tutengeneze mipango,tutengeneze michoro na hatua zote tumekwisha kuzikamilisha na Tunatarajia mwezi March kumkabidhi Mkandarasi na ujenzi utachukua muda wa miezi 08 hadi 10 utakuwq umekamilika.

Pia ametoa wito kuwa Wizara haitolala hadi kukamilisha Maagizo ya Rais dkt.Samia Suluhu wa Ujenzi huo wa Ukumbi wa Arena nchini Tanzania.