Jumanne , 28th Apr , 2026

Mshambuliaji wa Manchester United, Benjamin Sesko, amempa sifa lukuki nahodha wake, Bruno Fernandes (31), akisema anastahili kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu wa Ligi Kuu England (2025/26).

Bruno Fernandez na Benjamin Sesko

Bruno amekuwa na msimu wa kipekee kwa kutoa pasi za mabao 19 msimu huu (anakikaribia rekodi ya EPL ya muda wote).

Sesko amekiri kuwa Bruno amekuwa mwalimu wake mkubwa: "Ninapata maelekezo mengi sana kutoka kwake mazoezini... anastahili kushinda."

Tangu Michael Carrick achukue usukani, Bruno amekuwa moto zaidi akihusika katika mabao 12 (mabao 3 na assist 9)