Shabiki aliyetembea kwa mguu kuiona Simba afaidika

Jumatatu , 8th Apr , 2019

Shabiki wa klabu ya Simba aliyetembea kwa mguu kutoka Mbeya hadi Dar es salaam kushuhudia mchezo wa Simba na TP Mazembe amepewa ofa na klabu.

Shabiki Ramadhan Mohamed

Shabiki huyo amepewa ofa ya kusafiri na timu hadi Lubumbashi kuishuhudia na kuisapoti timu yake itakapocheza mchezo wa marudiano wa hatua ya robo fainali na TP Mazembe wikiendi hii.

Shabiki huyo Ramadhan Mohamed aliitwa na viongozi wa klabu, wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na sekretarieti ambapo amehaidiwa kugharamiwa na klabu kwenda Lubumbashi kuangalia mchezo huo wa marudiano.

Katika mchezo wa awali uliofanyika Jijini Dar e salaam wikiendi iliyopita, Simba na TP Mazembe zilitoshana nguvu ya kutofungana bao lolote. Timu itakayoshinda mchezo huo itafuzu hatua ya nusu fainali ya Klabu Bingwa Afrika.