Jumatano , 14th Nov , 2018

Klabu ya Simba kupitia kwa msemaji wake Haji Manara, imesema maandalizi ya mchezo wao wa kirafikia dhidi ya Nyasa Big Bullets ya Malawi siku ya Ijumaa Novemba 16, 2018.

Wachezaji wa Simba Aishi Manula kushoto na Deogratus Munishi kulia.

Manara amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kwani watapata burudani kubwa licha ya wachezaji wengi kua kwenye timu za taifa lakini timu hiyo ina kikosi kipana kwa wachezaji waliobaki watawapa raha.

''Mashabiki wasiwe na shaka, Simba ina wachezaji wengi sana kiasi kwamba tuna uwezo wa kucheza mechi mbili muda mmoja na tukapata matokeo, kwahiyo ukiacha wachezaji walioko kwenye majukumu ya timu za taifa, waliobaki pia ni wakali'', amesema.

Manara amewataja baadhi ya wachezaji wanaoweza kutumika katika mchezo huo kuwa ni Deogratius Munishi, Mohamed Hussein, Asante Kwasi, Paschal Wawa, Yusuf Mlipili, Mohamed Ibrahim, Mzamirau Yassin, Said Ndemla, Macel Kaheza na wengine.

Manara amesema lengo la mchezo huo ni kujipima uwezo kuelekea mechi yao ya klabu bingwa Afrika dhidi ya Mbambane Swallows ambayo itapigwa jijini Dar es salaam kati ya Novemba 27 na 28.