
Simba SC itaingia kwenye mchezo na Majimaji, ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa 1-0 na Azam FC Jumamosi katika mechi nyingine ya ligi hiyo.
Kipigo hicho kiliipunguza kasi ya Simba SC katika mbio za ubingwa na kujikuta wakiwapisha kileleni mabingwa watetezi, Yanga ambao juzi walishinda 2-0 dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga.