Jumatatu , 18th Mar , 2019

Kumekuwa na mijadala mbalimbali kuhusu nafasi za vilabu vya Tanzania kufuzu michuano ya vilabu Barani Afrika baada ya Simba kufuzu hatua ya robo fainali.

Simba

Matumaini yamekuwa makubwa hasa baada ya Simba kuisaidia Tanzania kupanda katika daraja za Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF kwa upande wa vilabu hadi nafasi ya 12. 

Kabla ya msimu huu, Tanzania ilikuwa nafasi ya 26 na pointi zake 3 zilizotokana na Yanga kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho, 2016 na 2018. 

Kufuzu kwa Simba robo fainali msimu huu, kumeipatia Tanzania pointi 15 ambapo zikichanganywa na zile 3 za Yanga, inakuwa na pointi 18.

Kufuzu kwenye hatua ya makundi ni pointi 0.5 na kufika robo fainali ni pointi 3. Simba imefika robo fainali msimu huu 2018/19 ambao thamani yake ni pointi 5. Maana yake ni 3×5=15.

Pointi hizi 15 zikijumlishwa na zile 3 za Yanga, Tanzania inakuwa na pointi 18. Hata hivyo pointi hizi zitaingia kwenye mahesabu kuanzia msimu ujao kwa ajili ya matumizi ya msimu wa mbele yake, yaani 2020/2021.

Kwa ilivyo hadi hivi sasa, Tanzania inafuzu kuingiza timu mbili katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika na timu mbili kwenye Kombe la Shirikisho katika msimu wa 2020/ 2021 isipokuwa endapo Gor Mahia ikifuzu hatua za mbele zaidi katika Kombe la Shirikisho au Simba ikishindwa kufuzu nusu fainali ya Klabu Bingwa Afrika.

Kenya ipo nafasi ya 14 katika mpangilio wa ubora uliotolewa, ambapo ina jumla ya pointi 14.

Bonyeza hapa chini kutazama zaidi.