Jumanne , 12th Feb , 2019

Baada ya kuchaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi Januari, kocha wa kikosi cha KMC, Etienne Ndayiragije, amesema kuwa malengo yao mwaka huu ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu bara.

Benchi la ufundi la KMC. Wa kwanza kushoto ni kocha mkuu Etienne Ndayiragije.

Etienne amesema, anayoimani na kikosi chake ambacho kwa asilimia kubwa kinaundwa na vijana, huku akiweka wazi kuwa timu hiyo itawashangaza wengi hasa kutokana na malengo makubwa waliyojiwekea msimu huu.

Aidha kocha huyo amekanusha vikali taarifa ambayo ilikuwa ikimuhusisha kuhitajika na klabu ya Simba, kwenda kukaimu nafasi ya kocha mkuu ambayo iliachwa wazi na Mrundi Masoud Djuma.

Kikosi hicho kutoka mitaa ya Kinondoni, kimeendelea kufanya mazoezi makali kuelekea mchezo ujao dhidi ya Kagera Sugar, utakaopigwa Ijumaa ya wiki hii kwenye uwanja wa Uhuru.

KMC imekusanya jumla ya alama 37, baada ya kushuka dimbani Mara 25, ikiwa imejikita kwenye nafasi ya tano, nyuma ya pointi 21 dhidi ya kinara Yanga mwenye pointi 58.