
Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, Stephen Ally amesema, Sserunkuma anatarajia kurejea nchini hivi karibuni kwa ajili ya kujiunga na timu na kuendelea na mazoezi ya Ligi kuu Soka Tanzania Bara.
Ally amesema, timu imeshaondoka hii leo kuelekea jijini Tanga kwa ajili ya kujiandaa na mechi dhidi ya Mgambo itakayochezwa Jumatano ya wiki hii, Uwanja wa Mkwakwani jijini humo.