Simba yaaga rasmi Klabu Bingwa Afrika

Jumamosi , 13th Apr , 2019

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wametolewa rasmi katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kukubali kichapo ugenini dhidi ya TP Mazembe.

Simba

Mchezo huo uliopigwa mjini Lubumbashi, umeshuhudia Simba ikipoteza kwa mabao 4-1, mabao ya TP Mazembe yakifungwa na Kabaso Chongo katika dakika ya 23, Meshack Elia dakika ya 38, Tresor Mputu katika dakika ya 62 na Jackson Muleka katika dakika ya 74 na bao pekee la Simba likifungwa na Emmanuel Okwi mapema katika dakika ya 2.

TP Mazembe imefuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo kwa uwiano wa mabao 4-1, baada ya mchezo wa mkondo wa kwanza kumalizika kwa sare ya bila kufungana Jijini Dar es salaam.

Pia TP Mazembe imefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya Klabu Bingwa Afrika kwa mara ya 12 katika historia yao.