Jumanne , 14th Jun , 2022

Afisa mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa leo wameongozana na msanifu majengo (architect) kwa ajili ya kutembelea eneo la Bunju ili kukagua mipaka na eneo ambalo litatumika kwenye ujenzi kabla ya Ijumaa Bodi ya Wakurugenzi Simba kukutana

Afisa mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez akiwa na wakandarasi.

Barbara amefunguka hayo leo kwenye uwanja huo akiwa ameambatana na mkandarasi ambaye atasimamia uboreshwaji wa uwanja huo.

Akizungumza mara baada ya kuonyesha mchoro huo amesema ameshawakilisha kazi yake kilichobaki ni Bodi ya wakurugenzi wa timu hiyo kupitisha na mchakato kuanza.

“Tuna mpango wa kuboresha uwanja wa Mo Simba Arena, kuweka uzio na majukwaa ili watu wakija hapa wafurahie zaidi na tayari mchakato ya maboresho hayo umeanza kwa kukamilisha mchoro"

"Kazi ya bajeti tutapata kwa Architect lakini naona ikiwa chini ya Bilioni 2 kwa uboreshaji wa viwanja hivi vya mazoezi,"

“Mimi kama Mtendaji mkuu kazi yangu ilikuwa ni kutengeneza michoro nimeshakamilisha kazi iliyobaki ni kuwaachia bodi kutoa marekebisho au kutoa ruhusa kuendelea,” amesema Barbara Gonzalez