Jumatano , 28th Nov , 2018

Klabu ya soka ya Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi murua wa mabao 3-1 dhidi ya Mbabane Swallows katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam na kuweka matumaini ya kusonga mbele.

Meddie Kagere na John Bocco

Mchezo huo uliokuwa kwa upande wa Simba kwa kipindi kirefu ulimalizika huku mabao Simba yakiyofungwa na John Bocco katika dakika ya 8 na 32, bao la tatu lililofungwa na Meddie Kagere katika dakika ya 84 na Clatous Chama katika dakika ya 90+2 huku bao pekee la Mbabane Swallows likifungwa na Guevane Nzambe katika dakika ya 24.

Simba inaungana na Mtibwa Sugar ambayo ilishinda mabao 4-1 kwenye mchezo wake wa kombe la shirikisho Novemba 27 jijini Dar es salaam katika harakati za kuhakikisha zinasonga mbele na kuiwakilisha vyema Tanzania.

Baada ya matokeo ya mchezo huo, sasa Simba inajiwekea matumaini makubwa ya kusonga mbele katika hatua ya pili huku ikisubiri  mchezo wa marudiano utakaofanyika wiki ijayo nchini Swartzland.