Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Simba yaivaa TFF sakata la pointi za Kagera

Jumatano , 19th Apr , 2017

Klabu ya Simba leo imeibuka na kupinga utaratibu unaotumiwa na TFF katika kushughulikia suala la pointi 3 ilizopewa kutoka klabu ya Kagera Sugar kwa kosa la kumchezesha mchezaji aliyekuwa na kadi 3, huku ikiituhumu TFF kuwabeba mahasimu wao, Yanga

Haji Manara - Msemaji wa Simba

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Manara, amesema wameshangazwa na kitendo cha Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji kupewa jukumu la kushughulikia maombi ya Kagera Sugar ya kutaka mapitio ya maamuzi ya Kamati ya Saa 72 kwani haina mamlaka hayo kwa mujibu wa utaratibu.

Manara amesisitiza kuwa lengo la TFF kulipeleka suala hilo kwenye kamati hiyo ni moja ya mbinu za kuhakikisha inaibeba Yanga katika mbio za ubingwa, na kwamba utendaji kazi wa kamati hiyo siku zote umekuwa si wa haki kwa upande wa Simba huku akikumbushia jinsi kamati hiyo ilivyoshughulikia sakata la usajili wa Ramadhani Singano 'Messi' wakati akitoka Simba kwenda Azam FC.

Akizungumzia jinsi kamati hiyo ilivyoshindwa kutoa maamuzi kuhusu pointi 3 za Kagera Sugar, Manara amesema Simba imeshangazwa na kitendo cha kamati hiyo kuwaita waamuzi wote hadi mwamuzi wa akiba wa mchezo  unaolalamikiwa kuwa mchezaji huyo alipata kadi ya njano kwa ajili ya mahojiano kwa gharama za TFF, lakini cha ajabu zaidi ni hatua ya kumuita hadi mchezaji mwenyewe anayedaiwa kupata kadi hiyo.

Mohamed Fakhi, Mchezaji wa Kagera anayedaiwa kuwa chanzo cha mgogoro

“Historically, haijawahi kutokea mchezaji aliyepewa kadi anaitwa kuhojiwa, yaani mwizi aliyeiba anaitwa kuhojiwa kama aliiba ndiyo kilichofanyika, sasa mwizi unamuita kumuhoji kama aliiba unataka akujibu nini?”. Alisema Manara

Aidha, Manara amesema Simba inapinga hatua ya kamati hiyo kulipeleka suala hilo polisi kwa kuituhumu Simba kughushi barua pepe iliyotumika kama ushahidi katika maamuzi ya awali kwa madai kuwa jeshi hilo liko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo Waziri wake ni Mdau wa Yanga, na kushauri kama wanaona barua ile imeghushiwa, wanapaswa waipeleke TCRA ambako ndiko kunahusika na mitandao.

Pamoja na hayo yote amemuomba Rais Magufuli kuingilia kati jambo hilo kwa kuwa mpira wa miguu umebeba dhamana kubwa kwenye mioyo ya watu pia kuwa na nguvu kubwa kuliko siasa kabla hawajaamua kufanya maamuzi mengine kutokana na kile wanachokiita kuwa ni hujuma wanayofanyiwa na TFF.

Celestine Mwesigwa - katibu Mkuu TFF

 

HABARI ZAIDI

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali

Daktari wa GGML aliyebobea katika magonjwa yatokanayo na kazi, Cretus Karwan akimpatia vipimo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la GGML na kupatiwa huduma za awali za upimaji wa afya katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Arusha.

Wananchi 200 wapimwa afya maonesho ya OSHA

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoka akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa masuala ya jamii na maendeleo ya kiuchumi kutoka GGML, Ruth Mharagi alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi jijini Arusha.

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu

Mwili wa Boaz Sanga, Mwanafunzi wa CHuo cha SAUTI Mwanza baada ya kupatikana Pembezoni wa Ziwa Viktoria

Mwanafunzi wa SAUTI afariki akijaribu kuogelea

Luteni Jenerali Charles Muriu Kahariri, CDF Mpya wa Kenya

Luteni Charles Muriu ateuliwa kuwa CDF mpya Kenya

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Taifa limejitosheleza kwa chakula kwa 124%

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda (Mwenye shati ya Bluu) akipata maelekezo wakati wa maonesho ya OSHA 2024 kwenye Viwanja vya General Tyres jijini Arusha.

RC ataka GGML iboreshe maisha ya wananchi Geita