Simba yajitoa michuano ya kimataifa

Ijumaa , 7th Jun , 2019

Timu ya Simba ambayo ndio inaongoza kwa kutwaa Kombe la Kagame mara nyingi zaidi kuliko timu yoyote, imetangaza kujitoa kushiriki michuano hiyo mwaka 2019.

Kocha Patrick Aussems na wachezaji wa Simba

Simba ambao wametwaa mara 6 miaka ya 1974, 1991, 1992, 1995, 1996 na 2002, imesema ratiba ya michuano hiyo inaingiliana na ratiba yao ya maandalizi ya msimu ujao wa 2019/20.

Simba ambao pia ni mabingwa wa kwanza wa kombe hilo lilipoanzishwa mwaka 1974, wamewataarifu mashabiki na wanachama wao kuwa hawatashiriki.

Watani wa jadi wa Simba, timu ya Yanga ya Tanzania, imetwaa kombe hilo mara 5 katika miaka ya 1975, 1993, 1999, 2011 na 2012.