Jumapili , 10th Aug , 2014

Uongozi wasema kutosikiliza ushauri kwa kocha Logarusic, kutokuelewana na baadhi ya wachezaji na kiwango kibovu cha timu hiyo ni baadhi ya sababu za timu hiyo kusitisha mkataba na kocha huyo ambaye alianza kazi hiyo hivi karibuni

Kocha mkuu wa Simba Mcroatia Zdravko Logarusic ametimuliwa rasmi hii leo.

Simba imemtimua kocha wake, Zdravko Logarusic ikiwa ni siku moja tu baada ya kufungwa mabao 3-0 na Zesco ya Zambia katika mechi ya siku ya Simba hapo jana mchezo uliofanyika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam

Rais wa klabu hiyo Evans Avevaamesema uamuzi huo wa uongozi wa Simba umefuatia timu hiyo kuonyesha kiwango kibovu kabisa katika mchezo huo na pia tabia ya kocha kutokua na maelewano na wachezaji ndipo uongozi wa Simba ukachukua uamuzi huo baada ya kikao cha majadiliano kwa takribani masaa matano

Tayari Simba imeanza kufanya maarifa ya kumpata kocha mpya ambapo tayari kuna taarifa zisizo rasmi za ujio wa makocha mzambia Patrick Phiri na Milovan Circovic ambao waliwahi kuinoa timu hiyo kwa nyakati tofauti

Aidha Aveva amesema kwa sasa timu hiyo itakua chini ya kocha msaidizi mzalendo Suleiman Matola mpaka hapo atakapopatikaan kocha mkuu mpya ambaye ameahidi atatua nchini muda wowote kabla ya ligi kuu kuanza.