Jumatatu , 17th Jan , 2022

Mabingwa watetezi wa Kombe la Azam sports federation, Simba SC wamepangwa kucheza na timu inayoshiriki ligi daraja la pili, Dar City FC katika hatua ya 32 bora ya michuano iyo.

Shirikisho la Soka nchini Tanzania ‘TFF’ pamoja na Wadhamini Wakuu wa Michuano ya Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ kampuni ya Azam Media, leo walisimamia shughuli za upangaji wa Ratiba ya hatua hiyo iliyofanywa kwa njia ya Droo katika Studio za Azam TV jijini Dar es salaam.

Droo hiyo iliwahusisha wachezaji wa zamani Abeid Mziba ‘Tekelo’ na Maalim Saleh ‘Romario’, Baraka Kizuguto (Afisa wa TFF) pamoja na mtangazaji Hassan Ahmed.

Simba wanatinga hatua hiyo baada ya kuifunga JKT Tanzania kwa 1-0 na kujiweka katika hatua sahihi ya kutetea taji lao ambalo wameshinda mara mbili mfululizo wakimfunga Namungo 2020 na Yanga SC mwaka jana.

Dar City FC, wakiwa wageni maskioni na machoni mwa watu huku heshima ya mashindano ikizingatiwa kutokana na maajabu ya FA.

2018/2019 Simba ilitolewa kwenye mashindano ya FA na Mashujaa kutoka mkoani kigoma kwa mabao 3-2 katika dimba la Benjamin Mkapa na hivyo kuhidhirisha maajabu ya kombe hili kuwa timu yoyote inaweza kutolewa ukiacha ukubwa na historia yao.

Mahasimu wao, Yanga SC wakiangukia kwa Mbao FC ya jijini Mwanza ambao walishuka daraja msimu wa mwaka 2018/2019 na sasa wakiwa Championship wakipambana kurudi ligi kuu.

Azam FC nao watakua nyumbani Azam Complex, Chamazi wakipapatuana na Transit Camp. 

Namungo FC nao wamepata nafasi ya kucheza mchezo wa hatua hiyo wakiwa nyumbani Mkoani Lindi ambapo wataikaribisha Lindi City.

Michezo mingine itahusisha, Polisi Tanzania  Vs Ndanda FC, Biashara United Vs Mbeya Kwanza, African Lyon Vs Kagera Sugar, KMC Vs Ruvu Shooting, Geita Gold Vs Tunduru Korosho.

Biashara Vs Mbeya, African Lyon Vs Kagera Sugar, Pamba FC Vs stand FC, Baga Friends Vs Catamine FC, Tanzania Prisons VS RHINO RANGERS, Coastal Union Vs Top Boys, Mbuni FC Vs Lipuli