Jumamosi , 20th Jul , 2019

Klabu ya soka ya Simba leo Julai 20, 2019, imeweka wazi michezo yake ya kirafiki itakayocheza ikiwa nchini Afrika Kusini.

Baadhi ya wachezaji wa Simba kwenye mazoezi nchini Afrika Kusini.

Simba ambayo imeweka kambi huko kwaajili ya maadalizi ya msimu ujao, itacheza mechi 4 dhidi ya timu za ndani na nje ya Afrika Kusini.

Ratiba hiyo inaonyesha Simba itakipiga na timu ya chuo cha ORBIT TVET ambacho kipo mjini Rustenburg walikoweka kambi yao. Mechi hiyo itakuwa Julai 23, 2019.

Kisha itacheza na Platinum Stars FC ya huko siku ya Jumatano ya Julai 24. Pia itacheza na Township Rollers ya Botswana Julai 27.

Mchezo wa mwisho utakuwa ni dhidi ya Orlando Pirates ambao utapigwa Julai 30, 2019.