Alhamisi , 9th Dec , 2021

Vilabu vya Tottenham Hotspurs na Leicester City vimekumbwa na janga la Covid-19 baada ya wachezaji na wafanyakazi wake 20 kukutwa na maambukizi ya ugonjwa huo kufuatiwa na ripoti iliyotolewa usiku wa jana leo nchini England.

(Kocha wa Spurs, Antonio Conte na baadhi ya wachezaji wa Leicester City)

Spurs ndiyo waliokuwa wakwanza kupata majanga hayo hadi kupelekea kambi yake ya mazoezi kufungwa Jumanne Disemba 7, 2021 baaa ya wachezaji wake kuonesha baadhi ya dalili hizo.

Majibu ya vipimo vya usiku wa jana vimeeleza kuwa, watu 13 kwenye timu ya Spurs wamepata maambukizi ya Covid-19, wachezaji 8 na wafanyakaz wengine 5 wakati Leicester City wamepata maambukizi ya wachezaji 7 na wengine 3.

Majanga hayo yametokea siku moja kabla ya Spurs kutaraji kucheza dhidi ya Rennes ya Ufaransa kwenye mchezo wa kuamua hatma ya kufuzu au kutofuzu hatua inayofuata ya mtoano kweny michuano ya Ligi ya Europa Conference leo

Mbali na mchezo huo ambapo wasimamizi wa michuano hiyo, Shirikisho la Soka barani Ulaya ‘UEFA’ limesema uchezwe lakini Spurs ana mtihani mzito kwani Jumapili ya Disemba 12 anamchezo wa EPL dhidi ya Burnley.

Kwa Upande wa Leicester, wamesafiri hadi Jijini Naples, Italy ili kucheza na Napoli kwenye mchezo wa mwisho wa kundi C wa michuano ya UEFA Europa League, bila ya wachezaji wake saba  na makocha watatu wenye Covid-19.