
(Kocha wa Brooklyn Nets, Steve Nash)
Nash ameyaongea hayo baada ya kupokea kipigo cha 5 katika michezo 15 ya mwanzo ya msimu huu mpya wa NBA licha ya kushinda michezo 10 na kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Eastern Conference.
Nash ameona pia kasi ya Golden State Warriors ambayo ni timu pekee iliyofungwa michezo michache, michezo 2 katika michezo 14 iliyocheza na pia kuwa timu pekee iliyoshinda michezo mingi, michezo 12 kwenye NBA.
Kwenye mchezo huo, Stephen Curry ameendelea kuwa miwba mchungukwa wapinzani baada ya kufunga alama 37, Assist 5 na rebound 7 huku Draymond Green akihakikisha Kevin Durrant aliyefunga alama 19 pekee.
Mpaka sasa Brooklyn wamepoteza dhidi ya timu zote zinatazamiwa kuwania ubingwa wa Larry O'Brien Trophy, timu hizo ni Miami Heats, Chicago Bulls and Milwaukee Bucks.