Jumatano , 13th Nov , 2019

Wikiendi hii kuanzia Ijumaa ya Novemba 15, 2019 Tanzania itakuwa kwenye vibarau viwili tofauti kwenye mchezo wa soka, ambapo timu zake za taifa za soka, ile ya wanaume (Taifa Stars) na ile ya wanawake (Kilimanjaro Queens zitakuwa zikiwakilisha nchi kimataifa.

Kushoto ni Gadiel Michael wa Taifa Stars na kulia ni wachezaji wa Kilimanjaro Queens.

Ijumaa timu ya taifa ya soka ya wanaume itakuwa dimbani kwenye uwanja wa taifa, kuivaa Equatorial Guinea, katika mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2021 nchini Cameroon. Mchezo huo utaanza saa 1:00 usiku.

Kwa upande mwingine timu ya taifa ya soka ya wanawake Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens itaanza kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la CECAFA, ambapo itafungua dimba na Sudan Kusini, mchezo ambao utapigwa kwenye uwanja wa Chamazi Dar es salaam.

Tayari timu za taifa kutoka mataifa shiriki zimeanza kuwasili nchini, ambapo timu za Taifa za Wanawake za Djibouti, Burundi na Kenya tayari zimeshawasili nchini tayari kwa michuano hiyo.

Michuano ya CECAFA kwa Wanawake inatarajia kuanza Novemba 16 mpaka Novemba 25,2019 Dar es salaam. Kilimanjaro Queens ndio mabingwa watetezi wakiwa wametwaa mara mbili mfululizo.