
Kocha msaidizi wa klabu ya Simba, Selemani Matola.
Akiongea mchana wa leo mbele ya wanahabri, Matola amesema “Kesho ni lazima tupate matokeo ili tusonge mbele, tumejipanga kupata matokeo. Tunamshukuru Mungu hakuna mchezaji ambaye tutamkosa, wote wapo kambini na hilo linatupa mwanga kuwa tunaweza kufanya vizuri”.
Nae nahodha wa kikosi hicho cha Wekundu wa msimbazi, John Bocco ajinasibu kufanya vizuri kwenye mchezo huo.
“Kwa upande wetu kama wachezaji tuko vizuri, tuna ari nzuri ya kuweza kupambana ili kufikia malengo ya timu yetu. Tumefanya maandalizi mazuri na tunaamini Mungu atatusaidia na tutafuzu hatua ya robo fainali”.
“Tuna wachezaji wenye uzoefu mkubwa na wanaoelewa kwanini wapo kwenye klabu. Tuko tayari”. Akamalizia, Bocco.
(Nahodha na mshambuliaji wa Simba, John Bocco.)
Ikumbukwa kuwa Simba ni kinara wa kundi A akiwa na alam 10 huku akihitaji alama 1 kutinga hatua ya robo fainali, Al Ahly ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 7, AS Vita ipo nafasi ya tatu ikiwa na alama 4 na endapo watapoteza mchezo huo watashindwa kusonga mbele sawa na Al Merrick mwenye alama 1.