Jumatano , 22nd Apr , 2026

Manchester United inamfuatilia kwa karibu Aurélien Tchouaméni kama mrithi anayewezekana wa Casemiro ambaye ni uhakika anaondoka Klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.

Aurélien Tchouaméni

Hata hivyo Klabu hiyo inamfuatilia kwa ukaribu kiungo wa Real Madrid Aurelien Tchouameni ambaye anaonekana ataweza kuziba nafasi ya nambari 6 Old Trafford. 

Hata hivyo, uhamisho huo utategemea sana mipango ya uhamisho ya Real Madrid ambapo Rais wa klabu Florentino Pérez anaaminika anamfuatilia kwa ukaribu Kiungo wa Manchester City Rodri.

Ikiwa Los Blancos watahitaji kubadilisha safu yao ya kati huku Eduardo Camavinga naye akitajwa kama mchezaji anayetarajiwa kuuzwa kunaweza kufungua fursa kwa United kufanya uhamisho wao.