Jumapili , 21st Feb , 2016

Timu ya Taifa ya walemavu ya Tanzania imefanya vyema michuano ya kufuzu Olympic itakayofanyika nchini Brazil, baada ya kushika nafasi ya pili huko Kenya.

Kocha Mkuu wa Timu hiyo Riziki Salum amesema timu hiyo imeonesha uwezo mkubwa kwa timu za wanawake na wanaume, kwa kuzifunga Misri, Ghana na Kenya.

Timu hiyo iliyokuwa na maandalizi ya kusuasua kabla ya kuondoka kutokana na ukosefu wa vifaa vya mazoezi, itasubiri pointi zitakazo tolewa na kamati ya kimataifa ya Olympic ili kushiriki mashindano ya Rio baadaye mwaka huu.

Timu ya tenesi ya walemavu mara kwa mara imekuwa ikilalamika vifaa kama viti vya magurudumu (Wheel Chair), ili kufanya mazoezi kwa ufanisi, na kufanya vizuri huko ni ushindi wa mchezaji mmoja tu.