Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

TFF yaitahadharisha Yanga vurugu uwanja wa Taifa

Jumapili , 26th Jun , 2016

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea taarifa juu ya mpango na kauli za baadhi ya viongozi wa Yanga kushawishi mashabiki wao kufanya vurugu dhidi ya warushaji matangazo ya televisheni ya moja kwa moja wakati wa mchezo wao Jumanne

Ofisi za makao makuu ya TFF Karume jijini Dar es Salaam.

Yanga imekuwa kwa nyakati tofauti ikipingana na maamuzi ama maagizo ya TFF, na sasa imeingia katika mvutano wa haki za matangazo baada ya awali juzi kupinga kuzuiwa kukaa uwanja mzima wakati wa mchezo wao wa kombe la Shirikisho la Afrika ngazi ya Makundi dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) utakaofanyika Juni 28, 2016 saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

TFF ikiwa msimamizi mkuu wa mpira wa miguu Tanzania, inawajibika na mara moja inachukua nafasi hii kuwatahadharisha baadhi ya viongozi wa Young Africans, wanachama na mashabiki wao kutofanya hivyo kwani itakuwa ni kinyume na kanuni za mashindano na mikataba ya udhamini katika hatua hii.

Ikumbukwe kwamba CAF inamiliki asilimia mia moja ya haki za habari na masoko katika ngazi hii ya makundi na jaribio lolote la kukwamisha matangazo ya biashara au utengenezaji na urushaji wa matangazo ya televisheni au ukwamishaji wa shughuli nyingine kama hizo kwa CAF au wakala aliyeteuliwa na CAF kutaigharimu klabu mwenyeji si kwa kutozwa faini tu lakini pia uwezekano wa kuondolewa mashindanoni.

Pia TFF inatoa tahadhari hiyo ikiwamo ile ya utamaduni wa kukaa uwanjani ili kuepusha aina yoyote ya vurugu kwenye michezo yake hususani hii ya hatua ya makundi.

TFF inafahamu kuwa tayari viongozi wa Young Africans walikwisha kusoma nyaraka na taarifa mbalimbali kuhusu kanuni na masuala ya udhamini kwa timu zinazofuzu hatua ya Nane Bora.

Wapenzi wa Yanga wanaombwa kufika kwa wingi na kuishangilia kwa nguvu timu yao ikiwa ni njia ya kuitia hamasa. Hata hivyo shamrashamra hizo zifanyike kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za mpira wa miguu na sheria za nchi.

Vitendo vya kuashiria vurugu na kufanya vurugu vikithibitishwa katika taarifa ya Mwamuzi, Janny Sikazwe wa Zambia; Kamishna wa mchezo, Celestin Ntangungira wa Rwanda na Mratibu Mkuu Maalumu kutoka Msumbiji, Sidio Jose Mugadza, hatua zake zitachukuliwa dhidi yake ikiwamo KUONDOLEWA KWENYE MASHINDANO.

Vilevile vitendo vya kutishia amani, kudhuru mwili au kuharibu mali vitachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za kijinai.

Katika mchezo huo wa kimataifa Na. 107, Mwamuzi Sikazwe atasaidiwa na Jarson Emiliano dos Santos kutoka Angola atayekuwa kwenye mstari wa kulia (line 1) na Berhe O’Michael wa Eritrea atakayekuwa upande wa kushoto (line 2) huku Wellington Kaoma wa Zambia akiwa ni mwamuzi wa akiba.

Wakati huohuo, kikao cha Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini kinatarajia kukaa siku ya Jumamosi tarehe 2 Julai 2016. Taarifa zaidi itatolewa karibuni.

HABARI ZAIDI

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Ajali yachukua uhai wa watu saba Morogoro

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wawekezaji wawekeze sekta za uzalishaji - Nchemba

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko

Serikali yaipongeza Red Cross

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja

Edgar Lungu, Rais wa Zamani Nchini Zambia Akitembea Kuzunguka Mji Mkuu wa Lusaka

Rais wa zamani Zambia Bw. Lungu hatarini kukamatwa

Mkuu wa Ulinzi Ukraine (Picha ya Website)

Zelensky amfukuza kazi mkuu wake wa ulinzi

Baadhi ya Wananchi wa Chindi na Ntinga wakiwa katika Harakati za Kuvuka Mto

Walazimika kulipa hadi 8000 kuvuka mto kwa mtumbwi