TFF yajibu kuhusu matumizi ya Bil 1 za Magufuli

Ijumaa , 15th Mei , 2020

Shirikisho la soka nchini (TFF) limesema Shilingi Bil 1 zilizotolewa na Rais Magufuli kwaajili ya maandalizi ya Fainali za AFCON U17 mwaka jana, hazikuingia kwenye akaunti ya TFF na wala wao hawajui zilitumikaje.

Makao Makuu ya TFF

Ufafanuzi huo umekuja mufa mfupi baada ya Mkurugenzi wa TAKUKURU Brigedia John Mbungo, kusema wanafanya uchunguzi juu ya matumizi ya fedha ndani ya Shirikisho la Soka zikiwemo hizo Bilioni moja.

Zaidi soma taarifa kamili hapo chini.