Hayo yameelezwa na Afisa wa Habari wa TFF Clifford Ndimbo wakati alipozungumza na mwandishi wa 'East Afrika Television' na kusema hawawezi kutoa maamuzi yeyote kwa sasa mpaka watakapo pokea ripoti kutoka kwa kamati husika zilizoundwa kushughulika na nidhamu kwa wachezaji.
"Sisi kwa upande wetu tunasubiri taarifa kama ilivyokuwa kawaida ya kanuni za mchezo kuwa ripoti itafikishwa kwa kamati husika ili waweze kuifanyia kazi na kama kutakuwa kuna chochote cha kipimo basi taratibu zitakuwa kama ilivyo kawaida", alisema Ndimbo.
Juma Said Nyosso alishikiliwa na Jeshi la Polisi jana (Jumatatu) muda mchache ilipomalizika mechi kati ya Simba na Kagera Sugar kwa tuhuma za kumpiga shabiki mpaka kumpoteza fahamu hapo uwanjani.



