
Mchezo wa gofu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Klabu hiyo Michael Luwongo alisema awali mashindano hayo yalipangwa yafanyike Juni 5 mwaka huu isipokuwa yalisogezwa mbele kutokana na kuingiliana kwa ratiba yao.
"Maandalizi ya mashindano yetu yanaendelea vizuri tunategemea mkuu wa Mkoa Amosi Makala atatufungia mashindano yetu hayo". amesema Luwongo.
Naye nahodha wa Klabu hiyo Japheth Masai alisema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na kuomba manahodha kutoka Klabu mbali mbali zitume majina ya wachezaji wao mapema.
'Katika mashindano hayo kuna zawadi mbali mbali ambazo zitatilewa kwa washindi tunaomba wadau mbali mbali wa mchezo huo wajitokeze katika mashindano hayo" amesema Masai.