Timu ya ligi kuu Afrika Kusini yafiwa na mchezaji

Jumatatu , 18th Mei , 2020

Mchezaji wa klabu ya Golden Arrows ya nchini Afrika Kusini Nkanyiso Mngwengwe mwenye umri wa miaka 30, amefariki Dunia asubuhi ya leo Mei 18, 2020 huko Durban.

Nkanyiso Mngwengwe enzi za uhai wake.

Kupitia taarifa ya klabu kwa umma, Golden Arrows imeeleza kupokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mchezaji huyo ambaye alijiunga na timu hiyo mwaka 2013.

Vyanzo tofauti tofauti nchini Afrika Kusini vinaeleza kuwa chanzo cha kifo chake ni shinikizo la moyo. 

Mwenyekiti wa klabu hiyo Ms. Mato Madlala ameeleza masikitiko yake na kutoa pole kwa familia ya Mngwengwe kwa kuondokewa na kijana wao, ambaye amemwelezea kama mtu aliyejitoa kwa kila hali kuitumikia timu hiyo.

Mngwengwe ameichezea mechi 140 timu hiyo ya Golden Arrows ambayo inayoshika nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi kuu msimu huu.

Chini ni taarifa ya Golden Arrows