Jumamosi , 9th Mar , 2019

Wakati Simba inaelekea kucheza mchezo wake wa 5 kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, kundi D leo Jumamosi Machi 9, dhidi ya JS Saoura, tayari baadhi ya timu zimefuzu robo fainali katima makundi mengine huku nyingine zikiaga michuano.

Espérance Sportive de Tunis.

Hiyo ni baada ya kundi B na C kucheza mechi zake ambapo mabingwa watetezi Espérance Sportive de Tunis maarufu ES Tunis, tayari wamefuzu robo fainali kwa kuongoza kundi B wakiwa na pointi 11 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine hata akipoteza mechi yake ya mwisho.

Katika kundi hilo Horoya inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 7 wakati Orlando Pirates ina pointi 6 huku FC Platinum ikiwa na pointi 1. Mechi za mwisho Horoya atakuwa nyumbani dhidi ya Orlando Pirates wakati FC Platinum ataikaribisha ES Tunis.

Katika kundi C, Ismaily ya Misri ambayo anachezea mchezaji Yahya Zayd, imeaga michuano hiyo baada ya jana kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na TP- Mazembe hivyo kubaki na pointi 2. 

Leo zitapigwa mechi za tano kundi A na kundi D ambapo kimahesabu Simba ipo njia panda ya kufuzu endapo itashinda huku AS Vita ambayo ipo nyumbani, kutoa sare au kupoteza dhidi ya Al Ahly. Tofauti na hapo Simba itasubiri mchezo wa mwisho dhidi ya AS Vita.

Misimamo ya Makundi mpaka sasa.

Group A
1. Mamelodi Sundowns 7
2. Wydad Athletic Club 7
3. ASEC Mimosas 4
4. Lobi Stars 4

Group B
1. Esperance 11
2. Horoya 7
3. Orlando Pirates 6
4. FC Platinum 1

Group C
1. CS Constantine 10
2. TP Mazembe 8
3. Club Africain 6
4. Ismaily 1

Group D
1. Al Ahly SC 7
2. Simba 6
3. JS Saoura 5
4. AS Vita Club 4