Henry Tandau - makamu wa Rais TOC
Makamu wa Rais wa Kamati ya Olimpiki nchini TOC Henry Tandau amesema, wao ambao ni wahusika wamejipanga kwa ajili ya kusaidia vyama ambavyo ndiyo vyenye michezo ili kuhakikisha vinatimiza malengo waliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kuitangaza nchi kupitia michezo.
Tandau amesema, kwa upande wa vyama vinatakiwa kukaa na kujitathimini ikiwa ni pamoja na kufanya maandalizi kwa ajili ya mashindano ya Olimpiki ikiwa ni pamoja na kuangalia michezo gani ina uwezo zaidi ya kufanya vizuri katika mashindano hayo.
Tandau amesema, vyama vingi huwa na maandalizi lakini katika kuangalia inatakiwa umakini kwani ipo michezo ambayo itaishia katika ushiriki wa Jumuiya ya Madola, mingine katika mashindano ya dunia na mingine katika Olimpiki.