'Tumuombee Samatta' - Waziri Mwakyembe

Jumanne , 21st Jan , 2020

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe amewataka Watanzania kumuombea Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta, ili aweze kufanikiwa katika klabu yake mpya ya Aston Villa ambayo amesaini mkataba wa miaka 4 na nusu.

Mbwana Samatta na Waziri Mwakyembe

Waziri Mwakyembe ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na EATV na EA Radio Digital ili kupata kauli ya Serikali kuhusiana na hatua aliyofikia Mbwana Samatta.

Mwakyembe amesema kuwa "hakika kama Serikali tumefurahi kama walivyofurahi Watanzania wote, tunampongeza sana Samatta kwa juhudi zake najua hakubahatisha, ila kwa nidhamu ya hali ya juu, na hiki ndiyo kinawakwamisha vijana wengi wa Kitanzania mtu akikupa safari mbili unajiona umemaliza." - Waziri Mwakyembe

Tazama video kamili hapo chini