Nyota wa zamani wa Ac Milan Andriy Shevchenko
Shevchenko mwenye umri wa miaka 45 ambaye ni mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2004 (Ballon D’or), video yake fupi ilioneshwa kabla ya kuanza kwa mchezo huo maarufu kama Derby Della Madonnina.
“marafiki zangu kutoka italia, tafadhali pazeni sauti zenu, watu wa Ukraine wanataka amani kwa sababu amani haina mipaka” amesema Shevchenko
Mchezo huo uliomalizika kwa suluhu ambapo sasa watarudiana tena mnamo jumatano ya April 20 huku nusu fainali ya pili ikitarajiwa kuchezwa leo baina ya klabu ya Fiorentina watakapowakaribisha kibibi kizee cha Turin Juventus majira ya 23:00 usiku katika uwanja wa Stadio Artemio Franchi


